NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Philipp Lahm ameondoa uwezekano wa kuitumikia tena timu hiyo baada ya kuamua kustaafu soka la kimataifa kufuatia ushindi wa Kombe la Dunia. Lahm alikongoza kikosi cha Ujerumani kilichokuwa chini Joachim Loew kwa taji la michuano hiyo walilochukua nchini Brazil majira ya kiangazi lakini kwa kuwashangaza wengi aliamua kutundika daruga zake na kuamua kuhamishia nguvu zake katika klabu. Nyota huyo ambaye anaweza kukaa nje ya uwanja mpaka machi mwakani kutokana kuumia kifundo cha mguu bado amesisitiza kuwa uamuzi aliofanya ulikuwa sahihi. Lahm amesema muda wake wa kuitumikia nchi hiyo umekwisha kwani hivi sasa atavaa ya Ujerumani akiwa mshabiki wakati akitizama mechi. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ameitumikia nchi hiyo kwa miaka 10 huku akipata nafasi ya kuwa nahodha na kuja kuw mabingwa wa dunia hivyo anadhani mafanikio hayo yanatosha.

No comments:
Post a Comment