Tuesday, December 2, 2014

BACH ASISITIZA OLIMPIKI YA MAJIRA YA BARIDI 2022 HAITAWEZA KUGONGANA NA KOMBE LA DUNIA LA QATAR.

RAIS wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, Thomas Bach amesisitiza kuwa hakutakuwa na mgongano kati ya michuano ya olimpiki majira ya baridi na michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar. Januari na Februari kipindi hicho ndio miezi inayofikiriwa kufanyika kwa michuano hiyo kwasababu ya joto kali lililopo Qatar majira ya kiangazi. Bach amesema alishahakikishiwa na rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter kuwa hakutakuwa na mgongano wowote. Bach ambaye ni raia wa Ujerumani amesema kutokana na hilo hana sababu yoyote ya kutomuamini Blatter. Toka Qatar kuteuliwa kundaa michuano hiyo ya mwaka 2022 kumekuwa mjadala wa muda muafaka wa kufanyika michuano hiyo kwani inaonekana haitaweza kufanya kama ilivyozoeleka katika miezi ya Juni na Julai.

No comments:

Post a Comment