Tuesday, December 2, 2014

NILIPONEA CHUPUCHUPU - WEBBER.

DEREVA mkongwe wa mashindano ya langalanga Mark Webber amesema upande aliogonga wakati anapa ajali katika mashindano ya Dunia ya Endurance ndio uliomsaidia kutopa majeraha makubwa. Webber mwenye umri wa miaka 38 alilazwa hospitali kwa siku moja baada ya kupata ajali hiyo katika mashindano hayo yaliyofanyika jijini Sao Paulo. Akihojiwa mkongwe huyo ambaye alistaafu rasmi mashindano hayo mwaka jana baada ya kupita miaka 12 amesema alikuwa mtu mwenye bahati kubwa kwani upande aliogonga haukuwa na madhara makubwa. Webber aliendelea kudai kuwa pamoja na kupata majeraha kadhaa lakini anadhani anaweza kushindana mwakani pindi atakapoalikwa.

No comments:

Post a Comment