MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amebainisha kuwa Mario Balotelli anaweza kuukosa mchezo wa muhimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Basel baadae leo kutokana na majeruhi. Liverpool ambao wana alama nne katika mechi tano wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Basel ya Switzerland katika mchezo wao wa mwisho wa kundi D ambapo watahitaji alama zote tatu kama watataka kusonga mbele pamoja na vinara Real Madrid katika kundi lao. Balotelli ambaye hajaonekana katika kikosi cha Liverpool toka wachapwe na Chelsea mabao 2-1 Novemba mwaka huu baada ya kupata majeruhi wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa anatarajiwa kuendelea kukaa nje tena katika mchezo wa leo. Akizungumza na wanahabari Rodgers amesema ana wasiwasi kama balotelli atakuwa fiti kwa ajili ya kucheza lakini tayari wana kikosi cha ushindi hivyo ni matumaini yao kitafanya kile wanachokitarajia.

No comments:
Post a Comment