Tuesday, December 9, 2014

PLATINI AMTOSA BLATTER.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini amekataa kumuunga mkono Sepp Blatter au mpinzani wake Jerome Champagne katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwakani, na kudai kuwa anatumaini ataibuka mgombea wa tatu katika kinyang’anyiro hicho. Akihojiwa na rekodi moja nchini Ufaransa, Platini amesema anadhani muda umefika kwa Blatter ambaye anagombea kwa kipindi cha tano toka ateuliwe kwa mara ya kwanza mwaka 1998, kuondoka. Platini amesema alimuunga mkono Blatter mwaka 1998 kwasababu alifikiri ni mtu sahihi kwa muda ule lakini baada ya vipindi vitano alivyoongoza anadhani ni muda muafaka wa kuleta mtu mwingine katika nafasi hiyo. Rais huyo wa UEFA aliendelea kudai kuwa taswira ya FIFA hivi sasa imeharibika vibaya kutokana na kshafa mbalimbali ndio maana anaona itakuwa vizuri kwa Blatter kuondoka lakini hadhani kama yeye mwenyewe anahitaji kuondoka. Akiulizwa nani atamuunga mkono katika uchaguzi huo, Platini amesema hana chaguo kwa wagombea wote wawili waliochaguliwa na akitemegea kujitokeza kwa mgombea mwingine katia uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment