Monday, December 15, 2014

CECAFA YAPANIA KUBADILI MFUMO WA MICHUANO YA CHALENJI.

BARAZA la Michezo la Afrika Mashariki na Kati-CECAFA limefuta rasmi michuano ya Kombe la Chalenji kwa mwka huu baada ya kushindwa kupata mwenyeji. Michuano hiyo inayoshirikisha nchi 12 ilikuwa imesogezwa mbele kutoka katika muda wake halisi ambao huanza Novemba 24 na kumalizika Desemba 6 kutokana na wenyeji Ethiopia kujitoa. Baada ya kuhaha huku na kule kutafuta mwenyeji mwingine hatimaye Katibu Mkuu wa CECAFA leo ameamua kuahirisha michuano hiyo kwa mwaka huu. Baraza hilo mbali na kusitisha michuano hiyo pia litaangalia utaratibu wa kutafuta mfumo mpya wa michuano hiyo ili kupunguza gharama na kuifanya kuwa tija zaidi.

No comments:

Post a Comment