MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Kobe Bryant amempita nguli wa zamani wa mchezo huo Michael Jordan na kukaa katika nafasi ya tatu katika orodha ya wachezaji waliofunga alama nyingi zaidi katika Ligi ya Kikapu nchini humo-NBA. Bryant mwenye umri wa miaka 36 alifikia mafanikio hayo wakati akiisaidia timu yake ya Los Angeles Lakers kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Minnesota Timberwolves. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Bryant amesema ni heshima kubwa kwake kufikia mafanikio hayo kwani ilikuwa safari ndefu. Bryant sasa anakuwa amepitwa na nyota wa zamani Kareem Abdul-Jabbar aliyefunga alama 38,387 na Karl Malone aliyefunga alama 36,928 wakati wakicheza enzi zao. Nyota huyo ambaye alifunga alama 26 katika mchezo wa Jana sasa amefikisha alama 32,310 katika mechi 1,269 alizocheza ukilinganisha na Jordan aliyekuwa na alama 32,292 katika mechi 1,072 alizocheza enzi zake.
No comments:
Post a Comment