Monday, December 15, 2014

LAHM ASISITIZA SCHALKE SIO YA KUDHARAU.

NAHODHA wa klabu ya Bayern Munich, Philipp Lahm amesisitiza kuwa hawapaswi kuidharau Shakhtar Donetsk ambao wamepangwa kucheza nao katika hatua ya timu 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika misimu mitatu mfululizo ya michuano hiyo Bayern imefanikiwa kuvuka zaidi ya robo fainali na Lahm amesema hawana mpango wa kutoka mapema mapema katika michuano hiyo. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo mara baada ya ratiba kutangazwa, lahm amesema anajua Donetski ni timu hatari lakini pamoja na hayo wanapaswa kuvuka hatua ya hiyo. Naye winga mahiri wa timu hiyo Arjen Robben naye alishukuru Bayern kuikwepa Arsenal lakini akaonya pia hawapaswi kuidharau. Katika misimu iliyopita Bayern wamekuwa wakikutana na Arsenal katika hiyo huku mara zote mbili wakifanikiwa kusonga mbele. Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya timu hizo utachezwa nchini Ukraine Februari 17 huku ule wa marudiano ukichezwa katika Uwanja wa Allianz Arena Machi 11.

No comments:

Post a Comment