MENEJA wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique amesema vilabu nchini Hispania vinapambana dhidi ya mashabiki wanaojaribu kufanya vurugu wakati wa mechi. Kauli hiyo ya Enrique imekuja kufuatia Lionel Messi kupigwa na chupa ya plastiki wakati akishangilia ushindi dhidi ya Valencia katika mchezo wa La Liga uliochezwa jana. Messi hakuumia katika tukio lakini Enrique amesema kinachotokea ndani ya uwanja kinaweza kuzuiliwa. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa unaweza kuwa na mtu yeyote ambaye anatamani kuanzisha vurugu lakini wanapamabna na kupinga matukio hayo.
No comments:
Post a Comment