KLABU kongwe ya Botafogo yenye maskani yake jijini Rio de Janeiro imeteremka daraja baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Santos jana. Ushindi huo wa Santos unaifanya klabu hiyo kuporomoka daraja kwa mara ya pili katika historia yake ya miaka 110 toka ianzishwe. Mara ya kwanza kushuka daraja kabla ya kupanda ilikuwa ni mwa 2003. Huku kukiwa kumebaki mechi moja kabla ya Ligi Kuu ya Brazil haijamalizika Botafogo wanashikilia nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa timu 20 wakiwa wamejikusanyia alama 33. Kabla ya mchezo wa jana Botafogo walikuwa wakihitaji alama sita ili kujinasua katika mstari wa kushuka daraja lakini kipigo cha jana kimefuta matumaini hayo. Klabu ya Cruzeiro ndio waliotawadhwa mabingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa pili mfululizo wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment