WINGA wa zamani wa klabu ya Liverpool John Barnes anaamini kiungo na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard, bado ana kiwango kizuri cha kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Barnes amesema katika umri aliofikia Gerrard anadhani bado ana ubora wa kutosha kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo. Barnes aliitumikia Liverpool kwa misimu 10 kabla ya kuondoka na kwenda kujiunga na Newcastle United katika umri kama aliokuwa nao Gerrard hivi sasa. Pamoja na ufanano wa umri ambao Barnes aliihama Liverpool, winga huyo anaimani Gerrard ana nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka atakapostaafu soka. Tayari Liverpool kupitia meneja wake Brendan Rodgers imetangaza kumpa ofa ya mkataba mpya Gerrard utakaomuwezesha kumalizia soka lake katika timu hiyo.

No comments:
Post a Comment