Tuesday, December 2, 2014

WACHEZAJI WA NFL WAUNGA MKONO MAANDAMANO YA FERGUSON.

WACHEZAJI watano wa Ligi ya Mpira wa Miguu wa Kimarekani-NFL huko St Louis wameingia uwanjani Jumapili iliyopita huku wakionyesha ishara ya mikono juu usifyatue risasi ambayo ndio imekuwa ikitumiwa na waandamanaji ambao wamekasirishwa na polisi katika kitongoji cha Feguson Darren Wilson kumuua kijana mweusi Michale Brown. Kwa mujibu wa ushuhuda uliotolewa mashahidi kuhusiana na sakata hilo walidai kuwa kijana huyo alinyoosha mikono juu kuashiria kutii amri lakini askari huyo mweupe alimfyatulia risasi na kumuua. Hatua hiyo iliyochukuliwa na wachezaji hao wa NFL inazua mjadala zaidi kuhusiana na sakata hilo pamoja na masuala mengine ya kibaguzi yanayoendelea nchini Marekani. Mmoja wa wachezaji walionyesha ishara hiyo Jared Cook amesema walifanya hivyo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na waandamanaji pamoja na watu ambao wamekuwa wakifanya kazi ngumu duniani kote.

No comments:

Post a Comment