Tuesday, December 2, 2014

NEWCASTLE YAPATA PIGO TENA.

GOLIKIPA wa klabu ya Newcastle United, Tim Krul anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na kupata majeraha ya kifundo cha mguu wakati akiwa mazoezini. Meneja wa klabu hiyo Alan Pardew amesema nyota huyo atakosa michezo mitano ya Ligi Kuu, na anatarajiwa kurejea tena uwanjani katikati ya mwezi Januari mwakani. Sasa Newcastle italazimika kumtumia golikipa wake namba mbili Rod Elliott kuziba pengo la Krul mpaka hapo atakapopona. Pardew amesema klabu hiyo itaendelea kuwakosa wachezaji wake wengine Siem de Jong, Ryan Taylor, Rolando Aarons, Mehdi Abeid na Fabricio.

No comments:

Post a Comment