MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amedai hana uhakika wakati gani Steven Gerrard ataisaini mkataba wake mpya lakini anaamini nahodha wake huyo bado ana ofa nyingi. Gerrard mwenye umri wa miaka 34 ambaye amepewa ofa ya mkataba mpya alifunga bao jana katika ushindi wa mabao 3-1 iliyopata Liverpool dhidi ya Leicester. Rodgers amesema kama ataweza kusimamia mazoezi yake na mechi anadhani anaweza bado akawa msaada mkubwa kwa kikosi chake. Akihojiwa kuhusiana na mkataba mpya Gerrard amesema ataamua kusaini pindi atakapokuwa tayari.
No comments:
Post a Comment