Wednesday, December 3, 2014

UFARANSA KUCHEZA NA BRAZIL UWANJA WALIOWATANDIKA 3-0 KATIKA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 1998.

SHIRIKISHO la Soka la Ufaransa-FFF limetangaza kuikaribisha Brazil katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Machi mwakani katika uwanja mbao waliifunga timu hiyo ya Amerika Kusini kw amabao 3-0 katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998. Mechi hiyo ya kirafiki itakayochezwa Machi 26 itakuwa ya kwanza kwa Ufaransa kwa mwakani wakati wakijiandaa na kuwa wenyeji wa michuano ya Ulaya taji ambalo walilichukua mwaka 1984 wakiwa wenyeji pia. Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo wakati wakinyakuwa taji la michuano hiyo mwaka 2000 ikiwa imepita miaka miwili toka watawadhwe mabingwa wa Kombe la Dunia kwa kuifunga Brazil atautumia mchezo huo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Denmark. Mechi hizo itakuwa sehemu ya ratiba ndefu kwa Ufaransa mwakani ambapo watacheza na Ureno, Serbia, Armenia na Uingereza.

No comments:

Post a Comment