MCHEZAJI nyota namba moja wa zamani katika mchezo wa gofu, Tiger Woods amesema bado anaweza kucheza katika kiwango cha juu, pamoja na kukiri kuwa haweza kwenda mbali kama wachezaji wengine wengi wa mchezo huo. Woods mwenye umri wa miaka 38 anatarajiwa kurejea tena mashindanoni katika michuano ya dunia itakayofanyika jijini Florida ikiwa ni ya kwanza toka Agosti apofanyiwa upasuaji wa mgongo. Akihojiwa nyota huyo amesema miaka yake ya kung’aa imeshakwisha kwani hawezi tena kushindana na vijana wanaochipukia ila anaweza kushinda pamoja na umri mkubwa alionao. Woods amefanikiwa kushinda mataji 14 makubwa ya gofu akiwa na umri wa miaka 32 pekee huku akifukuzia kufikia rekodi ya Jack Nicklaus aliyeshinda mataji 18 makubwa.
No comments:
Post a Comment