Wednesday, December 3, 2014

KOCHA WA TORINO AFUNGIWA MECHI MOJA, MANCINI APEWA ONYO.

MENEJA wa klabu ya Torino ya Italia Giampiero Ventura amefungiwa mechi moja kwa kosa la kuwaangalia mashabiki kwa nia ya kuwatishia. Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Italia imedai kuwamwishoni mwa mchezo wa Jumapili iliyopita ambao Torino walifungwa mabao 2-1 na Juventus, Ventura aliwageukia mashabiki kwa ishara ya hasira na kutishia. Kwa upande wa mwingine kamati hiyo pia iliiadhibu faini ya euro 15,000 klabu ya Sampdoria kwasababu ya mashabiki wake kuimba nyimbo za matusi wakati wa mchezo baina yao na Napoli uliomalizika kwa sare ya bao 1-1. Kocha wa Inter Milan Roberto Mancini yeye alipewa onyo baada ya kutolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo dhidi ya As Roma Jumapili iliyopita ambao walitandikwa kwa mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment