Wednesday, December 3, 2014

CONFEDERATION CUP: AL AHLY WAWEWESEKA KABLA YA MCHEZO WAO DHIDI YA SEWE SPORT.

KLABU kongwe ya Al Ahly ya Misri imefanya makosa ya aibu kwa kuchanganya utaifa wa wapinzani wao Sewe Sport katika tiketi ya fainali ya mkondo wa pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho. Al Ahly inatarajiwa kuwa wenyewe wa timu hiyo kutoka Ivory Coast Jumamosi hii katika Uwanja Cairo katika fainali ya pili ya michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza waliokutana huko Abidjan. Klabu hiyo yenye maskani yake jiji Cairo imechapisha tiketi 25,000 kwa ajili ya mchezo huo wa fainali lakini maofisa walioshughulika na suala hilo wakaitaja klabu hiyo ya Sewe Sport kuwa inatoka DR Congo badala ya Ivory Coast. Pamoja na makosa hayo kuna taarifa kuwa tiketi hizo zitakwenda sokoni hivyohivyo kwani hazitaweza kurekebishwa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment