NAHODHA wa timu ya taifa ya kriketi ya Australia, Michael Clarke amebubujikwa na machozi wakati akitoa heshima zake kwa rafiki ya mchezaji mwenzake Phillip Hughes katika mazishi yake. Hughes mwenye umri wa miaka 25 alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupigwa na mpira kichwani wakati wa mchezo wa kriketi jijini Sydney. Kifo chake kimehuzunisha wengi Australia na mazishi yake yamerushwa moja kwa moja katika luninga na kutizamwa na mamilioni ya watu katika luninga kubwa zilizowekwa katika miji mikubwa. Jumla ya watu wapatao 5,000 ndio waliohudhuria misa ya mazishi ya Hughes katika mji wa nyumbani kwao huko Macksville, New South Wales. Mazishi hayo pia yalionyeshwa moja kwa moja katika Uwanja wa Kriketi wa Sydney ambapo Hughes alipata majeraha Novemba 25 na kufariki siku mbili baadae akliwa hospitali.
No comments:
Post a Comment