Tuesday, December 9, 2014

GRANT AANZA KIBARUA GHANA.

KOCHA wa mpya wa timu ya taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars, Avram Grant anatarajiwa kukutana na wachezaji wa timu hiyo nchini Italia ukiwa ni mwanzo wa kibarua chake hicho huku mojawpao ya wachezaji hao akitajwa kuwa Michael Essien. Grant atakutana na wachezaji hao kwa mazungumzo kabla ya kuanza kambi yake rasmi ili kujiwinda na michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta mapema mwakani. Kocha huyo anatarajiwa kukutana na nahodha Asamoah Gyan kwanza kabla ya kuelekea nchini Italia kumuona Kwadwo Asamoah ambaye ni majeruhi. Mkutano wake na Michael Essien ndio utakuwa muhimu zaidi kwani kiungo huyo wa AC Milan anaungwa mkono sana na mashabiki nyumbani kwao huku pia akitarajiwa kukutana na rahman Chibsan, Emmanuel Agyemang Badu, Afriyie Acquah pamoja na Richmond Boakye Yiadom. Kocha huyo anatarajiwa kurejea Ghana kabla ya krismasi ili kuweka mipango yake ya maandalizi kabla ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment