Sunday, December 14, 2014

IRAN KUCHEZA NA TAIFA STARS MECHI YA KIRAFIKI.

SHIRIKISHO la Soka la Iran, limetangaza kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo itaweka kambi yake nchi Afrika Kusini huku wakicheza mechi tatu za kirafiki ili kujiandaa na michuano ya Kombe la Asia mwezi ujao. Kocha wa timu hiyo Carlos Queiroz ambaye aliivusha katika mzunguko wa pili katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil amechukua jumla ya wachezaji 21 katika safari yake hiyo. Katika kambi hiyo ya wiki mbili, Iran inatarajia kucheza mechi za kirafiki na Afrika Kusini wenyewe, Guatemala na Tanzania kabla ya kurejea Iran na kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Palestina Desemba 28 mwaka huu. Michuano ya Kombe la Asia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 9 mwakani huku Iran ikipangwa kucheza na Bahrain, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE katika hatua za makundi.

No comments:

Post a Comment