KAMISHNA wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani-MLS Don Garber amemuonya David Beckham kuwa kunatakiwa kuonekana ishara za maendeleo ya timu anayotaka kuanzisha huko Miami. Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza mwenye umri wa miaka 39, alikataliwa mipango yake ya kujenga uwanja wenye uwezo wa kubeba mashabiki 25,000 katikati ya mji wa Miami katika majira ya kiangazi mwaka huu. MLS inatarajia kupokea ripoti kutoka kwa kamati ya ligi hiyo mwishoni mwa wiki hii na Garber amedokeza kuwa baadhi ya maamuzi yatafanywa mapema mwakani. Akizungumzia ucheleweshwaji wa maendeleo ya timu ya Beckham, Garber amesema suala hilo haliwezi kuendelea hivyo kwani inabidi apande maendeleo yake haraka.
No comments:
Post a Comment