Wednesday, December 3, 2014

HATMA YA ROONEY BADO MASHAKANI.

MENEJA wa klabu ya Manchester United amesema nahodha wake Wayne Rooney anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi leo ili kubaini ukubwa wa majeraha ya goti yanayomkabili. Rooney mwenye umri wa miaka 29 alikosa mchezo walioshinda mabao 2-1 jana dhidi ya Stoke City baada ya kupata tatizo hilo katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Hull City. Akihojiwa Van Gaal amesema wanasubiri vipimo alivyofanyiwa ili kubaini ukubwa wa tatizo lake. Toka kuanza kwa msimu United imekuwa ikisumbuliwa na majeruhi huku wachezaji wengi wakiwa kutoka kikosi cha kwanza ambao wamekosa mechi nyingi muhimu mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment