MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza mbio za ubingwa wa Ligi Kuu bado hazijaisha pamoja na Chelsea kuanza vyema msimu huu. Chelsea iliyoko chini ya Jose Mourinho kwasasa haijafungwa na wadau wamekuwa wakianza kukifananisha na kikosi cha Arsenal ambacho kiliwahi kumaliza msimu bila kufungwa. Klabu ya Manchester City kwasasa wako nyuma ya Chelsea kwa alama sita na Wenger amesema kuna timu kadhaa ambazo bado zitaendelea kuwafukuza vinara hao kwa mechi zilizobaki. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa haiwezekani kudai mbio za ubingwa zimekwisha baada ya kuchezwa mechi 13 au 14 hivyo anaamini bado ubingwa uko wazi.
No comments:
Post a Comment