MENEJA wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ana uhakika Eden Hazard hivi karibuni atasaini mkataba mpya na kuendelea kubakia Stamford Bridge. Hazard amekuwa katika mazungumzo na klabu hiyo toka Juni na yuko tayari kusaini mkataba mpya ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo. Nyota huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Paris Saint-Germain msimu uliopita lakini wakati akizungumzia mipango ya kikosi chake Mourinho ameweka wazi kuwa hana shaka juu ya mustakabali wa mshambuliaji huyo. Mourinho amesema ukiangalia kikosi chake wachezaji wake wengi wako chini ya miaka 30 ukimuondoa Didier Drogba na John Terry ndio maana anataka kuendelea nao ili waweze kujiimarisha zaidi.
No comments:
Post a Comment