Sunday, December 14, 2014

KHAN ATETEA TAJI LAKE, SASA AMTAKA MAYWEATHER.

BONDIA wa Uingereza Amir Khan amefanikiwa kutetea taji lake la uzani wa welterweight baada ya kumchapa kwa alama bondia Devon Alexander wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini, Las Vegas. Katika pambano hilo ambalo muda mwingi lilikuwa limetawaliwa na Khan, mpinzani wake huyo alitoa upinzani hafifu. Khan ambaye anasifika kwa wepesi wake wa kurusha makonde aliendelea kudhibiti pambano hilo ambapo mpaka mwisho majaji wote walimpatia yeye ushindi. Baada ya pambano hilo Khan alisisitiza mpango wake wa kupigana na Mayweather ambapo anashikilia mkanda wa dunia wa uzito huo.

No comments:

Post a Comment