KOCHA wa klabu ya Entente Setif ya Algeria Kheireddine Madoui amesema mabingwa hao wa Afrika hawataidharau Auckland City katika mchezo wao wa Klabu Bingwa ya Dunia. Setif na Auckland ya New Zealand zitakwaana nchini Morocco kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo. Auckland ambao ni mabingwa wa Oceania waliwatandika mabingwa wa Morocco timu ya Moghren Tetouan kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ulifanyika Jumatano iliyopita. Madoui amesema hawapaswi kabisa kuidharau Auckland kwani walicheza vyema dhidi ya Tetouan na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga. Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Setif pamoja na timu kutoka Algeria kushiriki michuano hiyo huku kwa upande wa Auckland hiyo ikiwa mara yao ya sita wakiipita Al Ahly ya Misri.
No comments:
Post a Comment