MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Raul amedai kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kuja kuwa mchezaji bora wa wakati wote. Raul ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya New York Cosmos ya Marekani anaamini Ronaldo na nyota wa Barcelona Lionel Messi kwasasa wako katika viwango sawa kama walivyokuwa nguli wa Brazil Pele na Diego Maradona wa Argentina. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Januari mwaka huu huku pia akiwa na nafasi ya kushinda tena tuzo hiyo mapema mwakani. Raul mwenye umri wa miaka 37 amesema anadhani Ronaldo yuko katika kiwango cha juu hivi sasa na kama akiendelea hivyo anaweza kuwa mchezaji bora wa wakati wote. Nyota huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa anadhani Ronaldo na Messi kwasasa ndio wachezaji bora katika historia ya mchezo huo lakini ni ngumu kubashiri katika soka mchezaji anayemzidi mwenzake.
No comments:
Post a Comment