Monday, December 8, 2014

MAJERUHI RODRIGUEZ KUMSHAWISHI ANCELOTTI KUSAJILI DIRISHA DOGO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amedai kuwa wanaweza kuingia katika usajili wa dirisha dogo Januari mwakani ili kujaribu kutafuta mchezaji atayeziba nafasi ya James Rodriguez ambaye ni majeruhi. Ancelotti amesema miongoni mwa wachezaji wanaowafukuzia ni pamoja na kiungo wa klabu ya Cruzeiro ya Brazil, Lucas Silva. Vipimo vimeonyesha kuwa Rodriguez ambaye aliumia katika mchezo wa La Liga Jumamosi iliyopita dhidi ya Celta Vigo, hataweza kucheza michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia baadae mwezi huu. Madrid imekumbwa na balaa la majeruhi katika safu yake ya kliungo hivi karibuni baada ya Luka Modric kutarajiwa kurejea Februari mwakani huku Sami Khedira akiwa hajulikani lini anaweza kurejea baada ya kuumia katika mchezo wa Kombe la Mfalme. Ancelotti alikiri kuwa wana mpango wa kumsajili Silva lakini yote hayo yatasubiri mpaka baada ya krismasi wakati watakapojua muda halisi ambao wataweza kuwakosa wachezaji walioumia.

No comments:

Post a Comment