Monday, December 8, 2014

NIGERIA BADO VIGOGO WA SOKA AFRIKA - HAYATOU.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, Issa Hayatou amesema kushindwa kwa Nigeria kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon hakujapunguza umuhimu wa nchi hiyo katika muundo wa soka la Afrika. Mabingwa hao watetezi wa Afcon hawataweza kutetea taji lao hilo katika michuano hiyo itakayofanyika Guinea ya Ikweta baada ya kushindwa kufuzu katika mechi za makundi. Hayatou alimuambia rais wa Shirikisho la Nigeria-NFF, Amaju Pinnick kuwa familia nzima ya soka barani Afrika imesikitishwa kwa kukosekana kwa Super Eagles katika michuano hiyo ya mwakani. Katika taarifa yake hiyo kwenda kwa NFF Hayatou aliendelea kudai kuwa Afrika nzima itasononeka kuwakosa kumkosa bingwa mtetezi lakini hilo halitaweza kubadilisha ukweli kuwa Nigeria bado ni timu kubwa katika soka la Afrika.

No comments:

Post a Comment