Monday, December 8, 2014

MECHI ZA SOKA ZITAKUJA KUCHEZESHWA DRONES HUKO MBELE - BACKENBAUER.

RAIS wa heshima wa klabu ya Bayern Munich, Franz Beckenbauer anaamini kuwa waamuzi watakuja kubadilishwa na ndege zisizokuwa na rubani uwanjani wakati teknologia itakavyozidin kuendelea kukua katika soka. Ligi Kuu ya Soka nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga imepitisha matumizi ya teknologia ya kompyuta katika msitari wa goli katika msimu wa 2015-2016 kufuatia mfumo huo kufanikiwa katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Backernbauer amesema kutokana na hilo anadhani hana waamuzi wanaweza kuondolewa katika siku zijazo wakati teknologia itakavyozidi kukua zaidi. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa tunaishi katika ulimwengu wa teknologia hivyo itakuja kufikia wakati hata waamuzi hawatahitajika na kazi yao itafanywa na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zitakuwa zikifuatilia matukio yote uwanjani.

No comments:

Post a Comment