Monday, December 8, 2014

FIFA YATUPILIA MBALI MALALAMIKO YA CITY.

SHIRIKISHO la Soka la Dunia-FIFA halitarajii kuchukua hatua zozote dhidi ya timu ya HNK Rijeka ya Croatia baada ya kutupilia mbali tuhuma za ubaguzi zililizotolewa na Manchester City katika mchezo wa kirafiki wa timu ya vijana chini ya miaka 21. Kocha wa timu hiyo ya vijana chini ya umri wa miaka 21 wa City Patric Vieira alikitoa kikosi chake uwanjani baada ya Seko Fofana mwenye umri wa miaka 19 kulalamika kufanyiwa vitendo vya kibaguzi katika cmhezo baina yao Julai mwaka huu. Katika tarifa yake FIFA wamedai kuwa hakukuwa na vielelezo vya kutosha ili kuanzisha uchunguzi wa tukio hilo. FIFA waliendelea kudai kuwa rais wa Shirikisho la Soka la Croatia Davor Suker na Patrick Vieira wote walitoa ushirikiano unaostahili kuhusiana na tukio hilo. Fofana alijiunga na City akitokea klabu ya Lorient mwaka 2013 lakini bado hajafanikiwa kuibuka katika kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment