KLABU ya Swansea City imetangaza kuikatia rufani kadi nyekundu aliyopewa golikipa wa Lukasz Fabianski wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham United jana. Golikipa huyo wa zamani wa Arsenal alitolewa nje katika dakika ya 68 katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Upton Park ambao Swansea walifungwa mabao 3-1. Lakini kocha wa Swansea Garry Monk amelalamika akidai kuwa golikipa wake huyo hakustahili kadi hiyo. Fabianski alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Chris Foy wa madai ya kumzuia Diafra Sakho kufunga bao kwa kumshika.

No comments:
Post a Comment