Tuesday, December 9, 2014

MAN UNITED YAANZA KUCHANGANYA.

KLABU ya Manchester United jana ilifanikiwa kukwea hado nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuitandika Southampton kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa St. Marys. Mshambuliaji nyota wa United Robin van Persie ndiye aliyeibuka shujaa katika mchezo huo baada ya kufunga mabao yote mawili. United sasa inakwea katika nafasi hiyo na kuwashusha Southampton waliokuwa wakishikilia nafasi hiyo mpaka nafasi ya tano katika msimamo wa ligi. Chelsea ndio vinara wa ligi hiyo wakifuatiwa na Manchester City huku West Ham United wao wakiwa katika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment