MABINGWA watetezi wa Kombe la FA Arsenal, wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Hull City katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo msimu huu. Mchezo huo utakuwa kama marudio kwani timu hizo mbili ndio zilizocheza katika fainali ya msimu uliopita katika Uwanja wa Wembley. Mechi hiyo ni kati ya nne ambazo itazikutanisha timu za Ligi Kuu katika ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa jana huku zingine zikiwa Burnley itakayoikarinisha Tottenham Hotspurs, West Ham United ikifuata Everton na Newcastle United nao wakiwa wageni wa Leicester City. Kwa upande mwingine Liverpool wao watakwaana na AFC Wimbledon wakati Manchester United ambao ni mabingwa mara 11 wa michuano hiyo wao wakitarajiwa kucheza na Accrington Stanley au Yeovil. Kwa upande wa vinara wa Ligi Kuu Chelsea wao watacheza na Watford huku Manchester City wao wakiikaribisha tmu ya daraja la tatu ya Sheffield United.

No comments:
Post a Comment