Tuesday, December 9, 2014

WENGER AWATAKA WANAOMKOSOA WSUBIRI MWISHONI MWA MSIMU.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewataka wale wanaomkosoa kufanya hivyo mwishoni mwa msimu baada ya kocha huyo kuzomewa kufuatia kikosi chake kuchapwa mabao 3-2 na Stoke City. Kipigo hicho cha Jumamosi iliyopita kimeiacha Arsenal katika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13 baada ya kuchezwa mechi 15. Hata hivyo, Wenger amesema bado ni mapema mno kukikosoa kikosi chake na kuwataka mashabiki kuwa watulivu kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray baadae leo. Wenger amesema anapenda watu wamkosoe pale msimu unapomalizika na sio baada ya mchezo mmoja wakati wanaposhikwa na hasira. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na kipigo hicho kidogo morali imepungua kwa wcahezaji wake lakini wakiwa wachezaji wa kulipwa wanapaswa kukubaliana na hali kama hiyo na kuangalia jinsi ya kupata alama muhimu katika michezo inayofuata.

No comments:

Post a Comment