POLISI nchini Argentina wamedai kuwa nahodha wa soka nchini humo amepigwa na kufariki dunia na timu pinzani pamoja na mashabiki baada ya kuzuka vurugu katika mchezo wa ligi daraja ya tatu nchini humo. Mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita kati ya Tiro Federal na Chacarita ambazo zote zinatoka katika mji wa Aimogasta uliopo kaskazini mwa Argentina, ulisimamishwa dakika 10 kabla ya muda wa kawaida kumalizika kwasababu ya mapigano baina ya wachezaji uwanjani. Baada ya mchezo kumalizika Franco Nieto mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni nahodha wa Tiro Federal alishambuliwa na watu kadhaa wakiwemo wachezaji kutoka timu pinzani, kocha msaidizi na kundi la wahuni waliovamia uwanjani. Kwa mujibu wa binamu wa mchezaji huyo, amesema walimvamia na kuanza kupimpiga mateke na ngumi huku akijaribu kujitetea lakini walimzidi nguvu kwa kumuumiza sana maeneo ya kichwani. Katika mechi za soka nchini Argentina limekuwa jambo la kawaida kwani matukio hayo yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara ambapo toka mwaka huu uwanze watu wapatao 15 wameshauawa nje ya uwanja kwa vurugu.
No comments:
Post a Comment