Thursday, December 4, 2014

.SEVILLA, BARCELONA ZAIFUATA REAL MADRID KOMBE LA MFALME.

KLABU ya Sevilla imeungana na mabingwa watetezi Real Madrid katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kuididimiza timu ya daraja la pili ya Sabadell kwa jumla ya mabao 11-2 katika mechi mbili walizocheza. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Octoba Sevilla waliishindilia Sabadell kwa mabao 6-1 kabla ya kufunga tena mabao 5-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa jana. Kwenye hatua ya timu 16 bora Madrid sasa wana uwezekano mkubwa wa kukwaana na mahasimu wao Atletico Madrid ambao nao waliifunga timu ya daraja la tatu ya Hospitalet kwa mabao 3-0. Kwa upande wa Barcelona nao wamefanikiwa kusonga mbele kwa kuitandika Huesca nayo ya daraja la tatu kwa mabao 4-0 huku kocha Luis Enrigue akiwapumzisha nyota wake akiwemo Lionel Messi na Neymar.

No comments:

Post a Comment