Friday, December 19, 2014

NEYMAR ANACHUANA NA MESI NA RONALDO KWA UBORA - CARLOS.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos amemmwagia misifa nahodha wa sasa Neymar akisisitiza kuwa sasa anashindana na Lionel Messi na Ronaldo akiwa kama mchezaji bora duniani. Neymar mwenye umri wa miaka 22 alipewa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil na kocha mpya Dunga ambapo tayari ameshaingoza timu hiyo kushinda mechi siita mfululizo toka baada ya Kombe la Dunia huku akifunga mabao saba. Nyota huyo alikuwa mchezaji pekee pekee wa Brazil kuwepo katika orodha ya wachezaji 23 waliotajwa kugombea tuzo ya Ballon d’Or na Carlos anaamini mshambuliaji huyo wa Barcelona ni mchezaji bora wa tatu kumuona msimu huu. Carlos amesema Neymar ni mchezaji wa aina yake kwani amezoea soka la Ulaya haraka tatizo kubwa ni kwamba Messi na Ronaldo wanaimarika kila siku hivyo kila Neymar akijaribu kuwakaribia wanamuacha tena.

No comments:

Post a Comment