Friday, December 19, 2014

HALI YA KIFAMILIA KATIKA VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA MADRID - PEREZ.

RAIS wa klabu ya Real Madrid, Flotentino Perez amesema meneja wa timu hiyo Carlo Ancelotti ametengeneza mazingira ya kifamilia katika vyumba vya kubadilishia nguo na suala hilo ndio chachu kubwa ya mafanikio msimu huu. Perez amesema Ancelotti ametua Madrid akiwa na uzoefu mkubwa kama mchezaji na kocha katika vilabu vya AC Milan, Juventus, Chelsea na Paris Saint-Germain. Rais huyo aliendelea kudai kuwa uzoefu wake huo umemfanya kutengeneza hali ya kifamilia sambamba na mbinu imara vitu ambavyo ndio vimekuwa muhimili muhimu kwa timu hiyo kwasasa. Madrid ambao wametinga fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, kesho wanakabiliwa na kibarua kingine wakati watakapochuana na San Lorenzo ya Argentina jijini Marrakech ii kuamua bingwa wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment