RATIBA ya michuano ya 30 ya Mataifa ya Afrika mwakani imepangwa rasmi jana huko jiji Malabo, Guinea ya Ikweta. Upangaji wa ratiba hiyo ya makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kupisha nchi hiyo kupata nafasi ya kujiandaa kuwa wenyeji baada ya Morocco kujitoa kwa kuhofia kusambaa kwa virusi vya Ebola. Katika michuano hiyo timu 16 zitashiriki huku kwa mshangao bingwa mtetezi akishindwa kutetea taji lake baada ya kutolewa katika hatua za kufuzu samba na Misri na Angola. Timu hizo 16 zimegawanywa katika makundi manne ambapo kundi A litakuwa na timu za Guinea ya Ikweta ambao ndio wenyeji, Burkina Faso, Gabon na Congo Brazzaville huku kundi B likiwa na timu za Zambia, Tunisia, cape Verde na DR Congo. Kwa upande wa kundi C ambalo linatabiriwa kama kundi la kifo kutakuwa na timu za Ghana, Algeria, Afrika Kusini na Senegal na kundi D litakuwa na timu za Ivory Coast, Mali, Cameroon na Guinea. Wenyeji Guinea ya Ikweta ndio watakaofungua dimba na Congo katika michuano hiyo itakayoanza Januari 17 na kumalizika Februari 8 mwakani.
No comments:
Post a Comment