WINGA wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Marco Reus ametozwa faini ya zaidi ya euro nusu milioni kwa kukutwa na hatia ya kuendesha bila kuwa na leseni zaidi ya mara moja. Reus mwenye umri wa miaka 25 anatuhumiwa kusimamishwa na polisi mara kadhaa huku akipewa adhabu kwa kuendesha kasi kwa matukio matano kuanzia mwaka 2011 kabla ya mamlaka husika haijagundua kuwa alikuwa akiendesha bila leseni. Waendesha mashitaka wa Dortmund wamedai kuwa adhabu ya faini ya euro 540,000 aliyopewa inahusiana na makosa aliyoafanya kuanzia mwaka 2011 mpaka Machi mwaka huu. Reus mwenyewe amekubali kosa alilofanya huku akidai haikuwa uungwana na kuomba radhi kwamba hatafanya kosa kama hilo tena.
No comments:
Post a Comment