Thursday, December 18, 2014

CHELSEA KUVAANA NA LIVERPOOL CURLING CUP.

VINARA wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Chelsea wanatarajiwa kukwaana na Liverpool katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi katika ratiba iliyopangwa jana. Mbali na mchezo huo nusu fainali nyingine katika michuano hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu za Tottenham Hotspurs dhidi ya Sheffield United. Sheffield ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza tayari wamefanikiwa kuzing’oa timu za Ligi Kuu wakiwemo Southampton na West Ham United kabla ya kukwaana na Spurs ambao ndio mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2008. Mechi za mikondo miwili zinatarajiwa kuchezwa kesho huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Machi mosi mwakani.

No comments:

Post a Comment