Thursday, December 18, 2014

UCHUNGUZI MPYA WAGUNDUA KUWA EBOSSE ALIPIGWA.

VIPIMO vipya vya uchunguzi vimedai kuwa mchezaji nyota wa kimataifa wa Cameroon Albert Ebosse alifariki nchini Algeria kwa kupigwa na sio kupigwa na kitu chenye ncha kali kama ilivyodaiwa hapo awali. Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie alifariki dunia Agosti mwaka huu baada ya timu yake kufungwa katika mchezo wa soka. Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na mamlaka za Algeria ulibaini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifariki dunia kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani. Lakini vipimo vipya vilivyofanyika kwa ombi la wanafamilia vimedai kuwa kifo cha Ebosse kimetokana na kushambuliwa kwa kupigwa ikihisiwa kuwa katika chumba cha kubadilishia nguo. Ripoti hiyo ya Andre Moune inadai kuwa Ebosse alijeruhiwa maeneo kadhaa katika mwili wake huku kukiwa na dalili za kupambana wakatyi akishambuliwa. Familia ya mchezaji huyo imesema itafikisha ushahidi huo mpya kwa Shirikisho la Soka la Cameroon sambamba na Shirikisho la Soka la Afrika kwa ajili ya hatua zaidi.


No comments:

Post a Comment