Friday, December 19, 2014

BALOTELLI ALIMWA FAINI NA FA.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile alichokiandika katika mitandao ya ya kijamii. Adhabu hiyo itamlazimisha nyota huyo wa kimataifa wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili hii katika mchezo ya Ligi Kuu. Mbali na adhabi hiyo Balotelli pia amelimwa faini paundi 25,000 huku akilazimishwa kuhudhuria kozi ya maalumu ya ushauri nasaha na elimu. Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi. Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia.

No comments:

Post a Comment