Friday, December 19, 2014

MAKAMU WA RAIS WA SAN LORENZO ATAMBA KUISHANGAZA MADRID.

MAKAMU wa rais wa klabu ya San Lorenzo ya Argentina, Marcelo Tinelli amedai kuwa pamoja na utajiri iliyonao Real Madrid na wachezaji wenye thamani kubwa lakini wamepanga kuwashangaza mabingwa hao wa Ulaya. San Lorenzo inatarajiwa kukwaana na Madrid katika mchezo wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia jijini Marrakech, Morocco kesho. Tinelli amekiri kuwa utakuwa mchezo mgumu sana kuwafunga mabilionea hao wa Ulaya lakini amesema katika soka lolote linawezekana hivyo hana shaka na kikosi chake kuushangaza ulimwengu. Tinelli aliendelea kudai kuwa kitu pekee anachohitaji ni kushinda mchezo huo dhidi ya Madrid jambo ambalo amedai linawezekana. Naye kiungo wa klabu hiyo Julio Buffarini ametamba kuwa wachezaji wote wako tayari kupambana na Madrid kufa na kupona kuhakikisha wanaibuka kidedea.

No comments:

Post a Comment