MENEJA wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman amedai kuwa mshambuliaji wake Jay Rodriguez anaweza kuwa amepona ndani ya wiki sita zijazo kufuatia majeruhi ya muda mrefu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua. Rodriguez mwenye umri wa miaka 25 alipata majeraha ya goti katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City uliochezwa Aprili mwaka huu msimu uliopita. Koeman amesema nyota wake huyo atachelewa kidogo kupona kama ilivyofikiriwa awali lakini ana matumaini kuwa atarejea akiwa imara zaidi. Southampton imekuwa ikisuasua katika mechi zake za hivi karibuni ambapo wamefungwa mechi tano ikiwemo ile ya bao 1-0 dhidi ya Sheffield United ya robo fainali ya Kombe la Ligi Jumanne iliyopita. Kwasasa Southampton wako katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13.
No comments:
Post a Comment