MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amekataa kuwakosoa wachezaji wake baada ya kushikwa koo na timu ya daraja la chini ya L’Hospitalet jana usiku. Baada ya kuichapa timu hiyo ya daraja la tatu kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mfalme ilitegemewa kuwa mabingwa hao wa La Liga wangeibuka na ushindi lakini hali ikawa tofauti. Pamoja na sare hiyo ya mabao 2-2 waliyopata, Simeone aliwakingia kifua wachezaji wake kwa kudai kuwa walicheza vizuri ingawa walijisahau kidogo katika kipindi cha pili na kujikuta mabao hayo yakisawazishwa. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mwaka huu wamepoteza mchezo mmoja dhidi ya Calderon, hivyo inaonyesha jinsi gani wachezaji wake wanavyojituma na ni matumani yake wataendeleaa kufanya hivyo. Jumapili hii Atletico watakuwa na kibarua kingine wakati watakaposafiri kuifuata Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga.
No comments:
Post a Comment