Friday, December 5, 2014

RONALDO AENDELEA KUZIKWAA TUZO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameendelea kupokea tuzo za heshima kutokana na kiwango bora cha ufungaji alichonacho. Nyota huyo sasa ametunikiwa tuzo ya Shirikisho la Kimataifa la Historia na Kumbukumbu za Soka baada ya kufunga mabao 69 katika mashindano yote akiwa na Madrid na timu yake ya taifa mwaka jana. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alipokea tuzo yake hiyo jana na haraka alituma picha kwa mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram. Ronaldo alituma picha hiyo na kuwashukuru watu wote ambao wamekuwa pamoja naye katika safari yake hiyo.

No comments:

Post a Comment