KLABU ya Liverpool sasa imethibitisha kuwa ujenzi unaweza kuanza Jumatatu ijayo kupanua Uwanja wa Anfield mpaka kufikia uwezo wa kuingiza mashabiki 53,500. Kampuni ya Michezo ya Fenway tayari imeshaandaa mpango huo ambao utagharimu kiasi cha paundi milioni 114. Uwanja huo ambao kwasasa una uwezo wa kuingiza mashabiki 45,000 unatarajiwa kuongezwa viti vingine 8,500 katika eneo la jukwaa kuu. Mpango huo ambao umekuwa ukipangwa kwa kipindi cha miaka, unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2016-2017.

No comments:
Post a Comment